Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

SIKU 13 YA 30

Hili ni neno kwako uliye na mali. Yesu anakuonya na kukuita! Kuna mtu aliyemjia Yesu kwa heshima ili apate kujua njia ya kupata uzima wa milele. Alikuwa na mali nyingi. Yesu hakutaka kumpendeza tu, bali kumpa jibu la kweli! Baada ya kuongea naye juu ya amri za Mungu, Yesu akatambua kuwa alikuwa anaitegemea na kuipenda mali yake kuliko Mungu. Kwa hiyo tunasoma katika m.21-22: Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi. Hivyo Yesu alimsisitizia amri kuu: Usiwe na miungu mingine ila mimi (Kut 20:3)! Je, hazina yako iko kwa Mungu? Zingatia Mt 6:19-21, Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz