Yesu AnanipendaMfano
Kwani Biblia Inasema
Kama Wakristo, tumechagua Biblia kuwa kipimo kisichobadilika kwa vyote tufanyavyo na kuamini kwa sababu Yesu alifanya hivyo. Lazima tusome na kuamini neno la Mungu ili kugunfua utambulisho wetu katika Kristo. Yesu alidai kwamba kila neno la Maandiko linadumu ulimwenguni—hata zaidi ya sayari ambayo tunaishi. Ni rahisi zaidi mbingu na dunia kupita, kuliko hata herufi moja ya sheria kufutwa. (Luka 16:17)
Neno la Mungu pia inatupa uvumilivu, hamasisho, na tumaini tunapomfuata Yesu katika ulimwengu uliovunjika. Unapomfuata Yesu na kuruhusu Neno la Mungu kukuumbua na kukuumba, itakujenga tena ili uweze kuendeleza shughuli zako katika kila hali: husiano zako, fikra zako, tabia zako, na machaguo yako.
Katika dunia inayotingizika, inayobadilika, hatari, na inayohangaisha, Mungu anataka kukuwezesha uwe thabiti. Hata zaidi ya hayo, Mungu ameweka kazi nzuri ufanye. Mungu anataka uzae matunda. Anataka kukufanya uwe mwanga gizani. Mungu atakutumia katika mazingira yako na maishani mwako. Atafanya hivi unapojitiisha kwa Neno la Mungu na kuliruhusu kukutakasa na kukuboresha.
Hauna mmoja wetu amekamilika. Unapopata sehemu ya maisha yako ambayo hujafika penye ulitaka kufika ama penye Mungu alitaka ufike, usitamauke. Ukipata dhambi mpya moyoni mwako ama ufunue mambo yasiyopendeza maishani mwako, usidon’t get depressed. Kila mradi wa urejesho una kazi unaoendelea, vilevile hakuna mfuasi wa Yesu aliyekamilika.
Neno la Mungu pia ni kama ramani. Nimegundua haya kuhusu ramani. Haijalishi iwapo unatumia ramani ya karatasi ama ya apu, unawaamini wale watu waliochora ramani ama kujenga apu. Na vivyo hivyo ndivyo Neno la Mungu. Kuna nyakati ambazo tunafikiri, ninataka kuenda kuelekea kulia, lakini Neno la Mungu linanielekeza kuenda kushoto. Unaweza kuamini neno la Mungu katika kila hali.
Ukristo na muhimu ambazo tumefafanua kupitia maneno ya wimbow Yesu Anipenda zinabadili maisha yetu ya sasa na ulimwengu. Mungu anapofanya mwelekeo wako upya, kupitia utiifu wako na nguvu ya Roho Mtakatifu, utaanza kuishi katika hali ya uumbaji wako wa kweli na kupata utimizo na dhamira ambayo Mungu amekupangia.
Je, una taratibu imara na yenye upatano wa kusoma Neno la Mungu? Kula kiapo leo.
Kuhusu Mpango huu
Ikiwa mtu angekuuliza, "Ninahitaji kuamini ipi ili niwe Mkristo?" ungemjibu vipi? Kwa kutumia maneno ya wimbo upendwao, "Yesu anipenda, kweli ninajua, kwani Biblia inasema”, mhubiri aliyekuwa mwanahabari anakusaidia kuelewa unachoamini na sababu. Mwandishi maarufu John S. Dickerson anafafanua imani za kimsingi za Kikristo kwa uwazi na uaminifu na kuashiria mbona imani hizi ni muhimu.
More