Yesu AnanipendaMfano
Kwa Nini Unafaa Kusoma Haya?
Yesu alitangaza, “Nilikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele” (Yohana 10:10). Yesu alikuja kupa roho zetu pumzi ya maisha. Alikuja kutupa pumzi ya maisha ya milele ili tuishi na Mungu mbinguni baada ya kuondoka dunia hii. Alikuja kuwapa kila atakayeamini na kupokea zawadi yake ya ya bure ya wokovu pumzi hii ya maisha.
Popote ambapo tupo mautini kwa sababu ya makosa yetu, Yesu anaingia ulimwenguni mwetu na kuturejeshea pumzi ya maisha. Binadamu wote—wa dini, imani, na asili zote—hatimaye wanatamani uhusiano ambao Yesu anatoa. Ili kutuokoa kutokana na hali ya dhambi, Mungu akajiingiza ubinadamu.
Kama Wakristo, huyu ndiye Yesu ambaye tumemwamini—si mtu mzuri tu aliye na jina Yesu ama dhana inayoitwa Yesu ama hata mwalimu anayehamasisha aliyeitwa Yesu. Tunamwamini Yesu aliye Mungu katika mwili wa mwanadamu, Masihi aliyekufa msalabani kwa ajili ya dhambi za dunia na alifufuka kutoka mautini.
Ingawa Wakristo wengi wanaelewa ukweli huu, tumaini langu ni kukusaidia kujibu swali, Ninaamini nini kama Mkristo? Kwa sababu tunaishi katika ulimwengu amabao watu wengi wanatoa maana ya Ukristo kulingana na maoni yao, tunahitaji kuelewa kwamba imani za kimsingi za Ukristo ni ukweli usiobadilika. Hizo ndizo masharti ambazo zinazotuwezesha kupokea msamaha na uzima wa Yesu. Masharti zilitolewa na Mungu, si binadamu. Hazibadiliki, na zinaweza kueleweka na kila mmoja wetu.
Chini ya kila nyumba imara, pana msingi usioonekana unaoshikilia uzito wa ujenzi wote. Somo hili linaaka imani za kimsingi za Ukristo wetu. Ukikosa mmojawapo wa imani hizi muhimu na nyumba yako ya imani itaegama ama hata kuporomoka.
Ya kuhimiza ni kwamba, ukiweka haya mafunzo muhimu ya Kikristo yawe msingi wa imani yako, na utaweza kuona Mungu akijenga maisha ya udhabiti na usanii. Neno la Mungu linafafanua ukweli huu wa kimsingi. Somo hili linakusaidia kukagua msingi wa unachoamini kama Mkristo—ili uweze kujenga maisha ya imani kuu. Tunakua kwa kuamini anachosema Mungu katika Neno lake kisha kutii. Mungu atuwezeshe tufike kikomo cha wakati wetu pamoja tukiwa na upendo zaidi kwa Kristo, uhakikisho zaidi kuhusu imani yetu, na nguvu zaidi ya kutii Mungu wetu mwema.
Unajibu vipi swali, "Unaamini nini kama Mkristo?"
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Ikiwa mtu angekuuliza, "Ninahitaji kuamini ipi ili niwe Mkristo?" ungemjibu vipi? Kwa kutumia maneno ya wimbo upendwao, "Yesu anipenda, kweli ninajua, kwani Biblia inasema”, mhubiri aliyekuwa mwanahabari anakusaidia kuelewa unachoamini na sababu. Mwandishi maarufu John S. Dickerson anafafanua imani za kimsingi za Kikristo kwa uwazi na uaminifu na kuashiria mbona imani hizi ni muhimu.
More