Yesu AnanipendaMfano
Zipi Muhimu?
Muhimu ni mafunzo za kimsingi za Kristo. Ondoa mojawapo, na nyumba ya Ukristo inaporomoka. Ni muhimu kwani ukipoteza mojawapo, unapoteza nguvu ya Kristo kukubadili. Kanisa ikipoteza mojawapo, inapoteza nguvu ya Mungu ya wokovu kubadili watu wake na jamii yake.
Neno la Mungu linatoa hizi dhana muhimu—Maandiko ni uti wa mgongo wa imani hizi. Kichocheo chetu ni kujua imani za kimsingi za Ukristo kwa sababu vita vinaendelea ili kushinda roho zetu. Vita hivi kati ya wema na uovu vinapiganwa katika ulimwengu wa dhana—Udhahiri wa imani zako ni ala itakayokuwezesha kutofautisha kati ya dhana njema na dhana zinazopotosha au kulaghai. Kwa sababu tunapata nguvu na uzima wa Kristo kupitia imani yetu, sharti imani zetu ziwe sahihi.
Mstari wa kwanza wa wimbo upendwao, “Yesu Anipenda,” inaonyesha dhana za kimsingi za Ukristo:
Yesu / Anipenda / Mimi / Kweli ninajua / Kwani Biblia inasema.
Ukristo ni rahisi katika kiini chake ikiwa tunajua maana ya maneno hayo. Tumia njia hii kuuelewa:
YESU—Ninachoamini kuhusu Yesu
Yesu ni Mungu kikamili na binadamu kikamili, Masihi.
PENDA—Ninachoamini kuhusu upendo wa Mungu, alivyothibiti msalabani
Yesu alikuja ulimwenguni kwetu kwa utume wa kuokoa. Alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na kufufuka kutoka mautini.
MIMI—Ninachoamini kujihusu
Kila mwanadamu ana utukufu—na pia ana uharibifu. Tumeumbwa kwa mfano wa Mungu lakini dhambi imetunajisi. Penye uovu imetufisidi, Yesu anaweza kuturejesha ili tuwe “kiumbe kipya.”
NINAJUA—Ninachoamini ili kuwa na uhakikisho kuhusu wokovu wangu
Hatuwezi kustahili wokovu, lakini lazima tutumie nafsi yetu kukiri uhitaji wetu (tubu), kubali Yesu kuwa Mungu, na kuamini kazi yake msalabani.
KWANI BIBLIA INASEMA—Ninachoamini kuhusu masharti ya Mungu kwa maisha yangu
Tunachagua Biblia kuwa kipimo kisichobadilika kwa yote tutendayo na kuamini kwani Yesu ni mfano wetu. Lazima tusome na kutii Neno la Mungu ili kutimiza utambulisho wetu katika Kristo.
Kwa kupitia vishazi vitano vya maneno ya wimbo huu, tunapata ala ya nguvu ya ukumbusho ya kubeba dhana muhimu za Ukristo popote tuendapo.
Sala: Fumbua macho na moyo wangu katika safari hii. Nisaidie kupokea ukweli huu kutoka Neno lako. Ninataka fikra zangu zigeuzwe. Nisaidie kuamini unachotaka niamini. Amina.
Kuhusu Mpango huu
Ikiwa mtu angekuuliza, "Ninahitaji kuamini ipi ili niwe Mkristo?" ungemjibu vipi? Kwa kutumia maneno ya wimbo upendwao, "Yesu anipenda, kweli ninajua, kwani Biblia inasema”, mhubiri aliyekuwa mwanahabari anakusaidia kuelewa unachoamini na sababu. Mwandishi maarufu John S. Dickerson anafafanua imani za kimsingi za Kikristo kwa uwazi na uaminifu na kuashiria mbona imani hizi ni muhimu.
More