Yesu AnanipendaMfano
Anapenda
Siku ya leo tunaangazia umuhimu wa matendo ya Masihi—Yesu Kristo—kwa sababu matendo yake yanaonyesha kiini cha upendo. Alipotoa maisha yake kulipia dhambi za dunia—kulipa adhabu ya dhambi zangu na zako. Kwa hivyo, ni nini maana ya kusema, “Yesu anipenda?” Neno “pendo” lina maana gani?
Yesu alitoa maisha yake msalabani kwa hiari ili kukuokoa kutokana na dhambi na mauti. Sasa maisha mapya yapo punde unapomwamini na kupokea zawadi lake la wokovu. Hii inamaanisha kwamba una:
amani penye wasiwasi ungekuwa utambulisho wako,
uhuru kutokana na haya penye hatia ungekuwa utambulisho wako,
uhuru kutokana na dhambi penye ingekuweka utumwani,
utambulisho wa ukamilifu wa kiroho (utakatifu)
asili katika familia ya Mungu badala ya kuishi peke yako,
na hakikisho kwamba unapendwa.
Hii inamaanisha kwamba unapendwa na mtu aliye na cheo juu zaidi, aliye mkuu zaidi katika ulimwengu wote. Na maana yake ni kwamba Yesu—ambaye ni Mungu—alithibitisha upendo wake kwako kwa mtindo wa kusisimua zaidi unaowezekana: alijitolea mhanga kwa hiari ili kukuokoa.
Unapothibitisha imani zako kuhusu upendo wa Mungu kwako, lifuatalo ni ombi wa kukusaidia kufanya imani yako kuwa ya binafsi kwamba Yesu aliwasilisha upendo wake kwako alipoteseka msalabani.
Yesu,
Ninachagua kupokea msamaha ambao umewezesha kwa kunifia msalabani. Ninaamini kwamba ulithibitisha upendo wako kwangu ulipolipa gharama ya kuniokoa. Asante kwa kuchukua dhambi zangu na kuziweka juu yako. Asante kwa kunifia. Asante kwa kutoa zawadi za msamaha, uzima wa milele, na uhusiano ufaao na Mungu. Yesu, ulithibitisha upendo wako kwangu kwa matendo. Nisaidie sasa nionyeshe upendo wangu kwako na matendo yangu. Amina.
Kwa hivyo, ni kitendo kipi cha kujitolea ni kikuu zaidi ili kuwasilisha upendo wa mwengine? Yesu alijibu swali hili. Alisema: “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu: wa mtu kufa kwa ajili ya rafiki zake” (Yohana 15:13). Yesu alipotamka kauli hii, alikuwa akitabiri atakachotenda msalabani: kufa kwa ajili yako, rafiki yake.
Upendo unajithibitisha kwa vitendo kwa muda, upendo ni wa dhati iwapo vitendo ni vya kujitolea mhanga. Unaonyesha wandani wako vipi kwamba unawapenda?
Kuhusu Mpango huu
Ikiwa mtu angekuuliza, "Ninahitaji kuamini ipi ili niwe Mkristo?" ungemjibu vipi? Kwa kutumia maneno ya wimbo upendwao, "Yesu anipenda, kweli ninajua, kwani Biblia inasema”, mhubiri aliyekuwa mwanahabari anakusaidia kuelewa unachoamini na sababu. Mwandishi maarufu John S. Dickerson anafafanua imani za kimsingi za Kikristo kwa uwazi na uaminifu na kuashiria mbona imani hizi ni muhimu.
More