Yesu AnanipendaMfano
Mimi
Ni jambo la ajabu kuwaza kuhusu ubinadamu ukitumia mwelekeo wa Mungu—mamia ya mamilioni wa watu wote wakichagua jambo hili ama lile kila siku. Mungu anaona mauaji. Anaona upelelezaji wa mihadarati. Anaona mjamzito anayevuta kokeni, anayeathiri kitoto chake. Anaona waume na kina baba wadhalimu ambao wanaathiri wale ambao wameumbwa kukinga. Anaona vita na ubaguzi wa rangi, upendeleo, na ukosefu wa haki.
Vile vile, kila siku, Mungu anaona mamilioni ya kina mama wazuri wakikumbatia watoto wao, wakiwaliwaza usiku. Anaona kina baba wenye upendo wakiwafunza mabinti zao kuendesha baiskeli. Anaona mashujaa wanaohatarisha maisha yao na kuacha starehe zao ili kuokoa wengine.
Mungu anapotazama fujo yote ya binadamu—mazuri na mabaya—anahisi vipi? Ninapendekeza kwamba swali hili moja—Mungu ananionaje?— linajibu maswali yote ya yanayohusu binadamu wote.
Mungu anaona mporomoko mtukufu ambaye anayotamani kuhuisha.
- Tukufu. Umeumbwa katika mfano wa Mungu. Una thamani na heshima ya kiasili na hakuna anayeweza kukunyang'anya.
- Mporomoko. Kama mimi na kila mtu utakayemkuta, maovu ya dunia yamekuharibu kwa kiwango fulani.
- Unastahili kuhuishwa. Mungu anatamani kukurudisha kwa umbo la awali. Anataka uishi maisha ya uhuru kutokana na uharibifu; kutokana na hofu ya kifo; uhuru kutokana na utengano, uchungu, uharibifu, na kila aina ya uovu.
Kila binadamu, hata iwapo ana kasoro, amepotoka, ama ni mwovu bado anaendelea kubeba alama ama madokezo ya utukufu wa asili ambayo Mungu aliwapa wanadamu wote.
Vilevile, kila binadamu, hata iwapo ana vipaji, ni mwadilifu, au ni mwema, bado ametiwa madoadoa na uovu uliojaza ulimwengu huu na dhambi ambayo sote tumechagua.
Katika Waefeso 2:10, Mungu anakuita kazi yake bora, poema ya kisanii; hilo ndilo neno la Kigiriki ambalo kutokana nalo waingereza wanapata neno “poem” yaani shairi. Peponi, sisi tunaomwamini Bwana atuhuishe tutaonyesha ung'aavu wake, tukitangaza kwamba Mungu ni mkuu zaidi ulimwenguni wote, tena ni Mwumbaji shupavu, na tena ni Mkombozi wa hatimaye, anahuisha yale ambayo uovu ulikusudia kuangamiza. Huu ndio utambulisho wetu katika Kristo.
Ni katika sehemu ipi ya maisha yako ambayo unafahamu zaidi hali yako ya 'uharibifu'? Ni katika sehemu ipi ya maisha yako unahitaji zaidi nguvu ya Mola ya 'kuhuisha' ili kukufanya upya?
Kuhusu Mpango huu
Ikiwa mtu angekuuliza, "Ninahitaji kuamini ipi ili niwe Mkristo?" ungemjibu vipi? Kwa kutumia maneno ya wimbo upendwao, "Yesu anipenda, kweli ninajua, kwani Biblia inasema”, mhubiri aliyekuwa mwanahabari anakusaidia kuelewa unachoamini na sababu. Mwandishi maarufu John S. Dickerson anafafanua imani za kimsingi za Kikristo kwa uwazi na uaminifu na kuashiria mbona imani hizi ni muhimu.
More