Yesu AnanipendaMfano
Yesu—Mungu Kikamili na Mwanadamu Kikamili
Yesu ni Mungu kikamili: “Hapo mwanzo kulikuwako Neno [Yesu], naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu” (Yohana 1:1). Yesu ni mwanadamu kikamili: “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu: ambaye alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mugu kuwa kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu. Tena alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti—mauti ya msalaba” (Wafilipi 2:5–8).
Umuhimu wa usahihi wa imani zetu za kimsingi si ili “tuwe sahihi” bali ni ili “tukubaliwe kuwa waadilifu” na Mungu. Vilevile, kama sharti waya wa umeme uingizwe kisahihi katika soketi ili ifanye kazi ifaavyo, lazima tujipange kulingana na ulimwengu ulivyo, kama vile Mungu anavyovifafanua.
Mtu akisema “Ni nani anayeweza kusema Yesu ni nani?” tunaweza kujibu na ukweli huu rahisi: “Mbona tusitumie Yesu mwenyewe? Pengine tunafaa kutumia maneno yake mwenyewe kujibu swali hilo.” Yesu alijibu swali hili kwa njia nyingi tofauti na kwa kutumia maneno na vitendo vingi. Wakati mmoja, Yesu aliuliza rafiki zake kumi na mbili wa karibu walioamini kumhusu.
Mjadala huu umeandikwa katika Injili ya Mathayo, sura ya 16. Yesu anawauliza, “Nanyi mwaninena kuwa ni nani?” (Mistari. 13–15). Wafuasi hawa walijua kwamba Yesu alidai kwamba alikuwa njia ya pekee ya mbinguni na uzima wa milele (Yohana 14:6). Walijua pia kwamba Yesu alikuwa na uwezo wa kutenda miujiza. Na walijua kwamba maelfu wa watu walikuwa wameanza kuamini kwamba Yesu ni Mungu.
Ni jambo la kuvutia kwamba katika mjadala huu Yesu anajiita “Mwana wa Adamu”. Matumizi ya cheo cha “Mwana wa Adamu” yanasisitiza kwamba Yesu ni binadamu kikamili. Pengine si kawaida kusisitiza jambo kama hilo—Tazama, mimi ni mwanadamu. Lakini ikiwa daima umekuwa Mungu mwenyezi mbinguni, na wakati huu upo Sayari Dunia kama binadamu, yamkini utasema, “Tazama, Mimi ni mwanadamu!” Yesu alipenda kujiita hivi sana.
Tukirudi kwa swali. Mfuasi wake Petro alijibu moja kwa mojay. Alimtazama Yesu ana kwa ana na kusema, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai” (Mathayo 16:16).
Mbona ni lazima imani zetu kuhusu Yesu viundwe katika umbo la mfano ambao Yesu alifafanua? Mbona tunahitaji kuwa sahihi katika imani yetu kumhusu Yesu?
Kuhusu Mpango huu
Ikiwa mtu angekuuliza, "Ninahitaji kuamini ipi ili niwe Mkristo?" ungemjibu vipi? Kwa kutumia maneno ya wimbo upendwao, "Yesu anipenda, kweli ninajua, kwani Biblia inasema”, mhubiri aliyekuwa mwanahabari anakusaidia kuelewa unachoamini na sababu. Mwandishi maarufu John S. Dickerson anafafanua imani za kimsingi za Kikristo kwa uwazi na uaminifu na kuashiria mbona imani hizi ni muhimu.
More