Yesu AnanipendaMfano
Ninajua haya
Wokovu si ujira wa kutia bidii au kufikia kiwango fulani: “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani—ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu—wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. ” (Waefeso 2:8–9). Kumwamini Yesu unaleta nguvu ya Mungu maishani mwetu na matokeo ni wokovu wetu: “Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye” (Warumi 1:16).
Je, umekuwa na wakati wa maamuzi ambapo ukachagua kujiaminia Kristo? Leo tunafafanua kuhusu amuzi la kumchagua Yesu awe Mwokozi, Mfalme, na Mkombozi wako na umuhimu wa kuwa na uhakika katika chaguo hilo. Kupokea zawadi yake ni rahisi kwani ni kusema na kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka mauti.
Hapa pana sala ya kuondoa ukweli huu kutoka kichwa chako na kuuweka moyoni mwako, kutoka ukweli unaojua na kuufanya uwe imani unayochagua. Maneno ya sala hayana uchawi, lakini dhana zilizoko katika ombi hili lina nguvu yote ya ulimwengu iwapo utayaomba kutokana na moyo wa unyenyekevu na imani kwa Muumba wako.
Yesu,
Naja kwako, Mungu mwenyezi, na ninakiri kwamba maisha yangu hayafikii kiwango. Nimetenda dhambi na kukukosea kwa njia nyingi. Yesu, ninakushukuru kwa kunifia msalabani kwa dhambi na makosa yangu. Leo ninakukubali uwe Bwana na Kiongozi wa maisha yangu. Ninatubu na kuacha ujeuri wangu. Ninakuamini na moyo wangu, na ninachagua kukufuata na maisha yangu. Ninataka kupokea zawadi lako la bure la wokovu. Bwana, nisaidie kuishi kama kiumbe kipya wakati huu. Ninaomba haya katika jina lako na nikiamini kazi yako, Yesu. Amina.
Punde unapoweka imani yako kwa Yesu, jambo la kimiujiza linatendeka nafsini mwako, maishani mwako, na katika maisha yako ya milele. Mungu anavunja minyororo yako ya dhambi. Anakuandalia pahali nyumbani mwake na kukuasili katika familia yake. Mungu ni Baba yako, na anakupenda. Una familia ya kiroho ya waumini wengine kutembea nawe na kukuhamasisha katika barabara unaoelekea mbinguni.
Umepokea mwaliko wa Kristo kujiunga na familia yake? Weka alama kwenye kalenda yako ili ukumbuke kwamba siku hii ndiyo siku ambayo ulihakiki!
Kuhusu Mpango huu
Ikiwa mtu angekuuliza, "Ninahitaji kuamini ipi ili niwe Mkristo?" ungemjibu vipi? Kwa kutumia maneno ya wimbo upendwao, "Yesu anipenda, kweli ninajua, kwani Biblia inasema”, mhubiri aliyekuwa mwanahabari anakusaidia kuelewa unachoamini na sababu. Mwandishi maarufu John S. Dickerson anafafanua imani za kimsingi za Kikristo kwa uwazi na uaminifu na kuashiria mbona imani hizi ni muhimu.
More