Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila AsubuhiMfano
![Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila Asubuhi](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F19381%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Uchungu Huzuia Kusikia
Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya (WAEFESO 4:31)
Uchungu ulioelekezewa Mungu ni kizuizi cha hakika kwa kusikia sauti yake. Wakati wowote uchungu unapojaribu kukushikilia, ukatae. Wakati mwingi, shetani hujaribu kutufanya tufikirie ni sisi peke yetu tulio na wakati mgumu. Sina maana ya kusikika kama ambaye sina huruma, lakini hata kama shida zetu ni mbaya vipi, kuna mtu ambaye zake huwa mbaya kuliko zetu.
Kuna mwanamke aliyenifanyia kazi ambaye mumewe alimuacha baada ya miaka thelathini na tisa ya ndoa. Alimwachia tu barua, na akaenda. Ulikuwa msiba kwake! Nilijivuna sana kwa ajili yake aliponijia baada ya wiki chache na kuniambia, “Joyce, tafadhali niombee nisije nikamkasirikia Mungu. Shetani ananijaribu sana kwamba nimkasirikie. Siwezi kumkasirikia Mungu. Ndiye rafiki peke yake niliye naye. Ninamhitaji!”
Uchungu ulikuwa umeanza kuota mizizi katika moyo wa rafiki yangu kwa sababu maisha yake hayakuwa yameenda jinsi alivyotaka. Tunapoumia mioyo, lazima tutambue kwamba kila mtu ana hiari huru na hatuwezi kudhibiti hiyo hiari huru- hata katika maombi. Tunaweza kuomba Mungu azungumze na watu huenda wakatudhuru; tunaweza kuomba awaongoze kutenda yaliyo mema bali si mabaya, lakini la msingi ni kwamba, lazima awaache kuchagua wanayotaka. Mtu akifanya uteuzi unaoumiza, tusimlaumu Mungu na kuwa na uchungu naye.
NENO LA MUNGU KWAKO LEO
Ukiumia, usije ukamlaumu Mungu kamwe. Ndiye rafiki mzuri sana uliye naye.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila Asubuhi](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F19381%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Ibada hii inatoa mawaidha mafupi, yenye kuwezesha ambayo yatakuhimiza na kukusaidia kupanga wakati na Mungu kipaumbele chako cha juu, kukuza hamu ya muda wa kila siku naye, kuelewa majibu yake kwa maombi yako, na kudumisha uhusiano wako huku ukitumia wakati wa kibinafsi zaidi na Mungu. Anza siku yako na mtu ambaye hakupendi tu bali pia ana majibu yote ambayo utawahi kuhitaji!
More
Tunapenda kuwashukuru Joyce Meyer Mawaziri kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/
Mipangilio yanayo husiana
![Ibada juu ya Vita vya Akilini](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F21337%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Ibada juu ya Vita vya Akilini
![Kuwa Karibu Na Mungu Kila Siku](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F26551%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Kuwa Karibu Na Mungu Kila Siku
![Soma Biblia Kila Siku 11/2020](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F22531%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 11/2020
![Upendo Wa Bure](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F26579%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Upendo Wa Bure
![Moyo - Neno La Mungu Hugeuza Moyo](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F22660%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Moyo - Neno La Mungu Hugeuza Moyo
![Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F26578%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?
![Soma Biblia Kila Siku Machi 2021](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F24503%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Machi 2021
![MWANGA Kuvutiwa Maishani Na Mwanga Ajabu Wa Mungu](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F21139%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
MWANGA Kuvutiwa Maishani Na Mwanga Ajabu Wa Mungu
![Soma Biblia Kila Siku Julai 2021](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F26577%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Julai 2021
![Soma Biblia Kila Siku 07/2020](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F20586%2F320x180.jpg&w=640&q=75)