Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila AsubuhiMfano

Kusikia Kutoka Kwa Mungu  Kila Asubuhi

SIKU 7 YA 14

Sali na Ushukuru

Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo (DANIELI 6:10)

Kutoa shukrani ni muhimu kwa kuweza kusikia sauti ya Mungu kwa sababu kama tu vile sifa na kuabudu, ni kitu ambacho Mungu huvutiwa nacho. Ni kitu ambacho Mungu anapenda, kitu ambacho hutia joto moyo wake. Wakati wowote tunapompa Mungu furaha hivyo, tunazidisha undani naye - na hilo linajenga uhusiano bora naye. 

Pia, tunapokuwa wenye shukrani, tunakuwa katika hali ya kupokea mengi kutoka kwa Bwana. Iwapo hatuna shukrani kwa kile tulicho nacho, kwa nini atupatie kingine ili tunung’unike dhidi yake? Kulingana wa Wafilipi 4:6, kila kitu tunachoitisha Mungu kinafaa kutanguliwa na kuambatishwa na shukrani- tunafaa kuomba na moyo wa shukrani kwa vile tulivyo navyo tayari na kumshukuru pia mapema kwa kusikia na kujibu maombi yetu! Haijalishi tunachoombea, lazima shukrani ziambatishwe nazo. Desturi nzuri ya kuanzisha ni kuanza maombi yetu yote kwa shukrani. Mfano wa hili utakuwa: “Asante kwa yote uliyoyafanya katika maisha yangu, Wewe ni mwema na ninakupenda na kukufurahia”.

Ninakuhimiza kutathmini maisha yako, kuzingatia mawazo yako na maneno yako, na kuchunguza iwapo unatoa shukrani. Je, wewe hunung’unika na kulalamika kuhusu vitu? Au umejawa shukrani? Ukitaka changamoto, jaribu tu kukaa siku nzima bila kutamka neno la malalamiko. Anzisha mwelekeo wa shukrani katika kila hali. Kwa kweli, kuwa tu mwenye shukrani kabisa- na utazame ukaribu wako na Mungu ukizidi huku akimwaga baraka tele zaidi. 

NENO LA MUNGU KWAKO LEO

Zungumza maneno ya kutoa shukrani- sio maneno ya malalamiko. 

Andiko

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Kusikia Kutoka Kwa Mungu  Kila Asubuhi

Ibada hii inatoa mawaidha mafupi, yenye kuwezesha ambayo yatakuhimiza na kukusaidia kupanga wakati na Mungu kipaumbele chako cha juu, kukuza hamu ya muda wa kila siku naye, kuelewa majibu yake kwa maombi yako, na kudumisha uhusiano wako huku ukitumia wakati wa kibinafsi zaidi na Mungu. Anza siku yako na mtu ambaye hakupendi tu bali pia ana majibu yote ambayo utawahi kuhitaji!

More

Tunapenda kuwashukuru Joyce Meyer Mawaziri kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/