Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila AsubuhiMfano
Yupo Kila Wakati
Hakika wenye haki watalishukuru jina lako, wenye adili watakaa mahali ulipo wewe (ZABURI 140:13)
Ukweli kwamba Roho Mtakatifu anaishi ndani yetu unathibitisha kutaka kwake kuwepo kila mara ili kuzungumza nasi na kutusaidia tunapomhitaji. Tunapoendelea kukua kiroho, tutajaribiwa, lakini Mungu ametupatia Roho Mtakatifu kutuwezesha kuyapinga na kufanya uteuzi mzuri badala ya mbaya.
Hata hivyo, hakuna binadamu mtimilifu na tutafanya makosa. Lakini msamaha wa Mungu upo kwa ajili yetu kupitia kwa Yesu Kristo. Kupokea huu msamaha hututia nguvu na kutuwezesha kuendelea kusonga mbele na Mungu. Huweka mioyo yetu katika amani pia, kutuweka huru, na kutusaidia kusikia sauti ya Mungu kwa uwazi.
Kuhisi kushindwa na kuhumika kwa kila kosa tunalofanya hutudhoofisha. Badala ya kutumia nishati yetu kuhisi vibaya dhidi yetu tunafaa kuitumia kuhakikisha kwamba mioyo yetu inawiana na sauti ya Mungu anapotuongoza katika nguvu zaidi na uhusiano wa ndani naye. Msamaha wake na uwepo wake upo kwa ajili yetu sisi kupitia kwa Roho Mtakatifu. Unapomtafuta Mungu leo, ninakuhimiza kupokea upendo na huruma zake. Mikono yake iwazi na anangoja kuwa na muda nawe.
NENO LA MUNGU KWAKO LEO
Kumbuka kwamba Roho Mtakatifu yupo kwa ajili yako kila mara.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Ibada hii inatoa mawaidha mafupi, yenye kuwezesha ambayo yatakuhimiza na kukusaidia kupanga wakati na Mungu kipaumbele chako cha juu, kukuza hamu ya muda wa kila siku naye, kuelewa majibu yake kwa maombi yako, na kudumisha uhusiano wako huku ukitumia wakati wa kibinafsi zaidi na Mungu. Anza siku yako na mtu ambaye hakupendi tu bali pia ana majibu yote ambayo utawahi kuhitaji!
More
Tunapenda kuwashukuru Joyce Meyer Mawaziri kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/