Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila AsubuhiMfano

Kusikia Kutoka Kwa Mungu  Kila Asubuhi

SIKU 8 YA 14

Kuomba Maombi ya Mungu

Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. (ISAYA 55:9)

Ninafikiri mojawapo ya sababu zinazotufanya wakati mwingine kuhisi kutoridhika katika maombi au kuhisi kwamba “hatukumaliza” kuomba kuhusu jambo ni kwa sababu tunatumia muda mwingi tukiomba tu maombi yetu. Lakini ninawaambieni kwamba, kuna njia iliyo bora, ya juu na kamilifu: kuomba maombi ya Mungu. Kusema ukweli, ikiwa ninaomba maombi yangu, ninaweza kuomba kuhusu kitu kwa dakika kumi na tano na bado nihisi sikumaliza; lakini iwapo naongozwa na Roho Mtakatifu na kuomba maombi ya Mungu, ninaweza kuomba kwa sentensi mbili na nihisi kuridhika kabisa

Nimepata kwamba nikiomba maombi yaliyoongozwa na Roho, mara nyingi huwa rahisi na mafupi kuliko vile yangu yangekuwa. Huwa ni ya moja kwa moja na yanayolenga kitu. Huwa ninaridhika kwamba kazi imekamilika nikiomba jinsi Mungu anavyotaka kuliko vile mimi ninavyotaka. Tukiomba tunavyotaka, huwa tunalenga kuombea vitu vya kimwili na hali, lakini tukiwa tunaongozwa na Mungu, tutajipata tukiombea vitu vya kudumu kama utakaso wa mawazo na nia zetu na uhusiano wa ndani na Mungu. Mwambie Mungu akufundishe jinsi ya kuomba maombi yake badala ya maombi yako na utafurahia maombi zaidi

NENO LA MUNGU KWAKO LEO

Omba maombi ya Mungu sio yako.   

Andiko

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Kusikia Kutoka Kwa Mungu  Kila Asubuhi

Ibada hii inatoa mawaidha mafupi, yenye kuwezesha ambayo yatakuhimiza na kukusaidia kupanga wakati na Mungu kipaumbele chako cha juu, kukuza hamu ya muda wa kila siku naye, kuelewa majibu yake kwa maombi yako, na kudumisha uhusiano wako huku ukitumia wakati wa kibinafsi zaidi na Mungu. Anza siku yako na mtu ambaye hakupendi tu bali pia ana majibu yote ambayo utawahi kuhitaji!

More

Tunapenda kuwashukuru Joyce Meyer Mawaziri kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/