Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila AsubuhiMfano

Kusikia Kutoka Kwa Mungu  Kila Asubuhi

SIKU 11 YA 14

Sifu hadi Kwenye Uwepo wa Mungu 

Ingieni malangoni kwake kwa kushukuru, nyuani mwake kwa kusifu, mshukuruni, lihimidini jina lake. (ZABURI 100:4) 

Zipo njia ambazo tunaweza kupatikana ili kusikia sauti ya Mungu na mojawapo ni kuingia katika ibada na sifa inayotoka moyoni na yenye kuheshimika. Mungu anapenda kudhihirisha uwepo na nguvu zake kwa watu wanaomsifu na kumwabudu kwa kweli. Na uwepo na nguvu zake zinapokuja, tunasikia sauti yake, tunaona miujiza, watu wanaponywa, maisha yanabadilishwa, na mabadiliko yanafanyika kutoka ndani kwenda nje. 

Si hilo ni mojawapo ya mambo unayotamani katika uhusiano wako na Mungu? Unapozungumza naye na kutafuta kusikia sauti yake, si sababu yako kuu ya kuomba huwa ni kupata aina fulani ya mabadiliko katika eneo fulani la maisha yako? Iwapo unamwambia akupe kazi mpya, hayo ni mabadiliko. Iwapo unaombea mpendwa kuja kumjua Bwana, hayo ni mabadiliko. Iwapo unamwambia Mungu akupe ufunuo unaomhusu na kukusaidia kukua katika ukomavu wa kiroho, hayo ni mabadiliko. Iwapo unamwombea kijana jirani yako kuacha kutumia madawa, hayo ni mabadiliko. Iwapo unamwomba Mungu akusaidie ili usiwe mwepesi wa kukasirika, hayo ni mabadiliko.

Chochote unachoombea, mojawapo ya njia nzuri za kuanza ni kwa sifa na ibada. Zitasafisha nia yako mbele za Mungu na kukutengenezea njia ya kusikia sauti yake na mabadiliko kufanyika.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO

Unapohitaji kusikia sauti ya Mungu, msifu na kumwabudu.  

Andiko

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Kusikia Kutoka Kwa Mungu  Kila Asubuhi

Ibada hii inatoa mawaidha mafupi, yenye kuwezesha ambayo yatakuhimiza na kukusaidia kupanga wakati na Mungu kipaumbele chako cha juu, kukuza hamu ya muda wa kila siku naye, kuelewa majibu yake kwa maombi yako, na kudumisha uhusiano wako huku ukitumia wakati wa kibinafsi zaidi na Mungu. Anza siku yako na mtu ambaye hakupendi tu bali pia ana majibu yote ambayo utawahi kuhitaji!

More

Tunapenda kuwashukuru Joyce Meyer Mawaziri kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/