Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila AsubuhiMfano

Kusikia Kutoka Kwa Mungu  Kila Asubuhi

SIKU 12 YA 14

Mungu Huwazungumzia Rafiki Zake 

Bwana akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo (MWANZO 18:17)

Pengine hakuna mwingine anarejelewa kama “rafiki ya Mungu” kama Ibrahimu. Huku Biblia ikimrejelea Daudi kama mtu “aupendezaye moyo wa Mungu” na Yohana kama “mfuasi ambaye yesu alipenda,” Ibrahimu ana heshima maalum ya kuitwa rafiki ya Mungu zaidi ya mara moja katika Biblia. 

Mungu alipoamua kuhukumu watu wa Sodoma na Gomora, alimwambia Ibrahimu alichopanga kufanya. 

Katika urafiki, watu huambiana wanachopanga kufanya. Kwa sababu Mungu alimchukua Ibrahimu kama rafiki yake, alimwambia alichokuwa akienda kufanya- vile tu utakavyomwambia rafiki yako unachotaka kufanya. Ibrahimu alivyosikia kuhusu uharibifu ambao Mungu alikusudia kuachilia dhidi ya Sodoma na Gomora, alikuja karibu na kumwuliza “Utaharibu pia wenye haki na waovu” (Mwanzo 18:23). Jinsi tu Mungu alivyomwambia Ibrahimu kuhusu mpango wake kwa sababu walikuwa marafiki, Ibrahimu “akaja karibu” na Mungu na akazungumza kwa uwazi na ujasiri kuhusu mipango yake- kwa sababu walikuwa marafiki. Walikuwa na uhusiano ambapo wangewasiliana kwa uhuru na kuzungumza kwa uwazi. Aina ya urafiki wa ndani ambao Ibrahimu alifurahia na Mungu ulitokana na uhakika wa upendo wa Mungu kwake. 

Mungu anataka kuwa rafiki yako pia- kuzungumza nawe na kusikiza unachomwambia. Anza leo kukubali upya kwamba wewe ni rafiki ya Mungu na kwa hivyo unaweza kumkaribia. 

NENO LA MUNGU KWAKO LEO

Anzisha uhusiano na Mungu ambao unaweza kuzungumza naye kwa uhuru na kumsikia kwa urahisi anapozungumza nawe.  

Andiko

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Kusikia Kutoka Kwa Mungu  Kila Asubuhi

Ibada hii inatoa mawaidha mafupi, yenye kuwezesha ambayo yatakuhimiza na kukusaidia kupanga wakati na Mungu kipaumbele chako cha juu, kukuza hamu ya muda wa kila siku naye, kuelewa majibu yake kwa maombi yako, na kudumisha uhusiano wako huku ukitumia wakati wa kibinafsi zaidi na Mungu. Anza siku yako na mtu ambaye hakupendi tu bali pia ana majibu yote ambayo utawahi kuhitaji!

More

Tunapenda kuwashukuru Joyce Meyer Mawaziri kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/