Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kukombolewa kwa ndotoMfano

Dreams Redeemed

SIKU 6 YA 7

“Unataka nini?” Mume wangu wa zamani aliniuliza swali hili wakati ndoa yetu inasambaratika. " Ninataka ufanye kitu ambacho hakuna mwanaume amewahi kukifanya...nataka unipiganie." Sauti yangu ilitetemeka kwa kulia.

Baadaye, nilipokuwa napitia changamoto za njia ya mzazi mmoja, nilihisi Mungu ananiuliza swali hilohilo, tena na tena. " Unataka nini?? Kwa miaka miaka mingi, sikupata jibu la kumpa. Inajalisha kweli nachotaka? Nilishangaa.

Nilificha shauku na matamanio yangu chini ya msemo wa maarufu, ambao unasikika vizuri, " Mapenzi yako, siyo yangu".

Ijapokuwa kujisalishwa kwenye mapenzi ya Mungu ni jambo jema, ilinichukua muda mrefu kutambua kwamba Mungu haangalii utii wangu - anataka moyo wangu. Hatafuti watumwa wanaotii amri kama wajibu na mapenzi yaliyokandamizwa, bali mabinti na wana wanaomwitikia kwa upendo na uhusiano wa karibu.

Nimewahi kusikia, “Kutamani ni kuzuri kwako Longing.  Ni mwangwi wa miujiza ijayo.”

Mungu anajali ndoto zetu. Anajali kutamani kwa mioyo yetu. Kama tukimruhusu, anatumia majira ya kusubiri kujenga imani yetu na kutuleta karibu naye tunaposhiriki matamanio yetu. Kushiriki ndoto zetu na Mungu haimani tunapata kila tunachohitaji. Yeye siyo jini letu. Lakini hatua tuu ya kushirikiana ndoto zetu na Mungu hutuleta karibu naye.

Unaweza kufikiria kuwa na rafiki au mwenza ambaye hajawahi kukuambia kuhusu ndoto na matamanio yake? Nadhani tutajisikia kwamba hakuna muunganiko kati yetu na uhusiano wetu utaonekana ni wa juu juu tu. Tabia ya kushirikiana mahitaji yetu na matamanio yetu huongeza uwezo wa ukaribu na Mungu na wengine.

Kwangu mimi, baada ya miaka ya kujaribu kukataa ndoto ya kukaa mezani na familia yangu mwenyewe, hatimaye nilimwambia Mungu kile nilichokitaka. Nilitaka kuolewa tena.Nilitaka mtu nitakayeweza kushirikiana naye ndoto na maono, wajibu na changamoto, kicheko, na machozi.

Majira ya kusubiri yaliendelea. Ndani yake, Mungu aliendeleza uponyaji wa ndani kwangu. Alitumia muda wa kusubiri kunifundisha juu ya kurudisha urafiki na ukweli wa mahusiano ya hisia za ndani yalivyo na watu salama. Pia nilikuw katika imani kwamba Mungu ni, hakika, mwema. Alinifundisha kwamba mazingira katika maisha yangu hayabadili ukweli huu. Alinifundisha kusimama katika ukweli huu, hata kama nilidhani sikuona ushahidi wake.

Unatakanini

Katika maandiko yote, Yesu anauliza maswali mbali mbali kwa watu aliokutana nao. Naamini anakuuliza pia na wewe. Nakutia moyo utafakari jibu la swali hili na ushirikiane naye. Anaweza kuaminiwa na matamanio ya moyo wako.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Dreams Redeemed

Tunafanyaje wakati ndoto zetu zinapoonekana kuwa haziwezi kutimia? Ukiwa umeshinda matusi na hofu, pamoja na kuvunjika moyo baada ya ndoa kuvunjika, ninakabiliwa na swali mara kwa mara. Ikiwa unapitia uharibifu wa tukio au hasara, au kuchanganyikiwa baada ya kusubiri jambo kwa muda mrefu, ndoto ya Mungu kwa maisha yako bado iko hai! Rafiki ni wakati wa kuwa na ndoto tena.

More

Tungependa kumshukuru Harmony Grillo (I Am A Treasure) kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: http://harmonygrillo.com