Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kukombolewa kwa ndotoMfano

Dreams Redeemed

SIKU 4 YA 7

Kukatishwa tamaa na maumivu yana njia ya kuchochea majaribu. Vinatuacha kuwa wahanga kwenye maeneo ambayo tuko dhaifu. Ikiwa ni kijitenga, kula kupita kawaida, kufanya ngono zembe, au kupata glasi chache nyingi za mvinyo, hamu yetu ya kupata usingizi, au kukwepa maumivu tunaamua kukubaliana na hali. Tunajiambia wenyewe tunastahili kujisikia bora zaidi.

Tunapoumia, ni rahisi sana kuachilia ndoto kwa kitu cha muda mfupi. Starehe ya mitego yetu inapendeza mwanzoni, yenye uharibifu mbaya zaidi.

Kuna onyesho katika onyesho la sinema maarufu, La Boehme ambapo wanaume wawili wanateseka na baridi kali ya Paris. Mmojawapo, mwandishi, ametumia muda mwingi kwenye kazi yake. Ameshikwa na baridi kiasi cha kushindwa kuzingatia uandishi wake tena.

Akiwa hana fedha ya kununulia makaa au kuni kuwashia moto, katika kipindi cha kukata tamaa, mwandishi anatupa kazi yake yote kwenye sehemu ya kuwashia moto. Ndani ya sekunde chache, makaratasi yake yote yenye maandishi yake yaligeuka majivu.

Mwandishi aliitoa ndoto yake, yote aliyoyafanyia kazi, kwa ajili ya kupata burudani kidogo ya muda. Alikubali.

Tunaona mfumo huohuo katika hadithi ya Esau katika kitabu cha Mwanzo. Akiwa amechoka, anarudi nyumbani anakutana na harufu ya dengu. Akihitaji kwa bidii kuishi, Esau anatoa uzaliwa wake wa kwanza, haki zote, mamlaka na urithi ambao uliambatana na mzaliwa wa kwanza, kwa ajili ya chakula. Alitoa baadaye yake kwa utoshelevu wa tumbo lake.

Sikilia, Ninajua.

Ninajaribiwa kula hisia zangu napokuwa nahuzunika ( Mara nyingi nakubali!). Baada ya talaka yangu, upweke ulinifanya nijaribiwe kushusha kiwango na kukubaliana na kuwa na mtu. Nashukuru, sikuingia kwenye jaribu hili, lakini ni wazi lilikuwepo.

Nilipokuwa napoteza nyumba yangu, na katika kuelekea kufilisika, jirani alinipa nafasi ya kazi ya kulipwa mshahara mkubwa wa tarakimu sita katika kuuza madawa. Nilijaribiwa kukubali ile kazi. Lakini kukubali hiyo kazi ilimaanisha kuiweka kazi ya hazina kwenye banda la nyuma. Faraja ya muda ya uimara wa kifedha haukuwa sababu ya kuachilia kusudi Mungu aliloniitia. 

Wakati mwingine ndoto ya Mungu inahitaji kujitoa. Kama ilivyo, Mungu anahusika sana na tabia yetu kuliko kiwango chetu cha faraja.

Tunaweza kuacha vitu vigumu vijenge tabia yetu au kuharibu. Tunaweza kuacha ndoto kwa kilicho cha muda, au tunaweza kuvumilia na kuruhusu uvumilivu kututia nguvu katika tabia yetu na kujenga ukomavu ndani yetu.

Usiache ndoto kwa kitu ambacho ni cha muda mfupi. Usiache maumivu au kukatishwa tamaa kukufanye upoteze ndoto yako kwa ajili starehe za kitambo. Usiache. Kuna mengi kwa ajili yako.

Kuna uhuru katika mwisho wa uaminifu wako.   Kwa ajili yako binafsi, na kwa watu wengine watakaoathirika na wewe wakiishi kikamilifu kwenye kusudi lako!

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Dreams Redeemed

Tunafanyaje wakati ndoto zetu zinapoonekana kuwa haziwezi kutimia? Ukiwa umeshinda matusi na hofu, pamoja na kuvunjika moyo baada ya ndoa kuvunjika, ninakabiliwa na swali mara kwa mara. Ikiwa unapitia uharibifu wa tukio au hasara, au kuchanganyikiwa baada ya kusubiri jambo kwa muda mrefu, ndoto ya Mungu kwa maisha yako bado iko hai! Rafiki ni wakati wa kuwa na ndoto tena.

More

Tungependa kumshukuru Harmony Grillo (I Am A Treasure) kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: http://harmonygrillo.com