Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kukombolewa kwa ndotoMfano

Dreams Redeemed

SIKU 5 YA 7

Asubuhi moja nzurimya Jumamosi, nilimwangalia binti yangu wa miaka 3 alipokuwa amelala kwa utulivu. Nilikuwa nasubiri kwa hamu sana aamke, kwa sababu nilikuwa nimepanga kumshangaza kwa mlo wa asubuhi anaoupenda sana na kumpeleka kuangalia sinema nje ya nyumbani na kupata ice cream.

Kwa taratibu nilisogeza nywele mbele ya paji lake la uso na kuanza kumpapasa mashavu. "Amka malalaji," nilimnong'oneza sikioni. 

Ghafla, mikono yake na miguu yake aliikunjua na kuirusha hewani. "Hapana! sitaki kuamka," alipiga kelele sana. Sura yake ndogo, ya kimalaika akageuka kuwa kukasirika na kuwa mwekundu.

Moyo wangu ulinyong'onyea. Mbali ya kukasirishwa na kukasirika kwake, nilivunjika moyo sana kwamba tusingekuwa na siku ya kufurahisha niliyotarajia kwa ajili yake.

Binti yangu alitaka kuendelea kulala, alipokuwa. Alikuwa ameridhika katika kulala kwake. Kukataa kwake kwa hasira kulimfanya akose nafasi ya kutoka kwa ajili ya kitu kikubwa. Haijalishi nitampeleka siku nyingine maalum na kumzawadia kwa hasira yake. Kama angejua nilichokuwa namtakia, angefanya tofauti? Kama aliuamini mpango wangu, kama aliniaminimimi, angeitikia tofauti?

Najiuliza kama nimewahi kukosa kile Mungu alichokuwa nacho kwa ajili yangu, kwa sababu nilichukuliwa sana na starehe niliyokuwa nayo nilipokuwa. Nikitilia maanani kile nilichokuwa nakitaka. 

Mara nyingine, tunataka tunachotaka, na kufikiria ndicho tunachokitaka. Lakini kama kweli tunaamini kwamba Mungu ni mwema na mipango yake ni mizuri, tutamsikiliza. Tutamfuata--hata kama inavuruga mipango yetu na kutuondoa katika hali ya kustarehe kwetu. Hata kama itamaanisha kwamba ni muda wa kuachia mahusiano, tabia, au maumivu ambayo yamekuwa yakituvuta nyuma. 

Tumaini liko katika msingi wa imani--kuwa na tumaini kwa Mungu ni kutumaini mpango wake, hata kama hatuuelewi. Pia ni msingi wa ndoto ya Mungu kwa ajili ya maisha yetu. Katika nyakati ambapo ilionekana kana kwamba kama maisha nilivyoyajua yalikuwa yanashindikana, tumaini katika Mungu lilinipa mahali imara pa kusimama. 

"Amka, mpenzi. Fungua macho yako. Nifuate. Nina mipango ya ajabu kwa ajili yako. Ili uweze kupata kile nilichokuwekea tayari, huwezi kukaa hapo ulipo. Ni wakati wa kusonga mbele, mpenzi wangu."

Naamini Mungu anakualika wewe na mimi katika mpango ambao ni wa ajabu zaidi ya mawazo yetu yanavyoweza kuelewa. Mpango ambao utajumuisha kurejeshwa na kukombolewa kwa vyote vilivyopotea na kuibiwa. Swali ni, tutamtumaini na kumfuata?

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Dreams Redeemed

Tunafanyaje wakati ndoto zetu zinapoonekana kuwa haziwezi kutimia? Ukiwa umeshinda matusi na hofu, pamoja na kuvunjika moyo baada ya ndoa kuvunjika, ninakabiliwa na swali mara kwa mara. Ikiwa unapitia uharibifu wa tukio au hasara, au kuchanganyikiwa baada ya kusubiri jambo kwa muda mrefu, ndoto ya Mungu kwa maisha yako bado iko hai! Rafiki ni wakati wa kuwa na ndoto tena.

More

Tungependa kumshukuru Harmony Grillo (I Am A Treasure) kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: http://harmonygrillo.com

Mipango inayo husiana