Kukombolewa kwa ndotoMfano
Siku yangu ya kwanza ya siku ya akina mama- siku ambayo nilidhani ningepokea maua mengi na salamu za upendo. Badala yake, nilijikuta nasikiliza ushuhuda ambao ungepelekea mwisho wa ndoa yangu. Nikiwa na huzuni na hasira, sikuwa katika hali ya kulea mwanangu kwa masaa 24 ya mwanzo. Marafiki zangu walikuwa wema sana kumchukua na kutoka naye.
Nilipofika kumchukua siku iliyofuata, nilikuwa nabubujikwa machozi sebuleni kwao, nikilalamika, " nilikuwa bibi harusi wake. Tulikula viapo. Tulitakiwa kulea watoto na kuwa na wajukuu pamoja. Tungevunja mnyororo wa kuvunjika ndoa kwenye familiamzetu. Tulitakiwa kuzeeka pamoja".
Alinisikiliza kwa makini kabla ya kusema chochote. " Harmony, inaoneka umekuwa na taswira ya ulivyotaka maisha yenu yawe. Ninajua ni ngumu, lakini itakuwa ni wakati wa kumkabidhi Mungu kitambaa na tumaini ili achore taswira mpya. ”.
Alikuwa sahihi. Sikuwa na nahuzunikia maisha niliyoyajua, lakini pia yale niliyoyafikiria tutakuwa nayo. Huzuni juu ya huzuni. Wengi wetu tumetumia muda kuweka taswira maisha yetu yatakuwaje. Tunachora vitambaa kwenye vichwa vyetu juu ya ndoa zetu, watoto wetu, kazi zetu, urafiki wetu, na wakati mwingine hata ratiba ya mambo yote haya.
Maono ni kitu chema, lakini nini kinatokea wakati ndoto zetu na matarajio yetu yanapovunjika kwa kukatishwa tamaa maishani mwetu? Kwa kifo cha mpendwa wetu, kuvunjika kwa ndoa, au kupoteza kazi? Tunapokeaje? Tunamkasirikia Mungu na kupokea kwa uchungu? Tunaahidi kutokuota tena, kwa sababu inaumiza sana kutumaini? Au, tuko tayari kuomba na mikono yetu ikiwa wazi na kujisalimisha kwake.
Nami pia nimekuwa na taswira ya jinsi maisha yangu yatakavyokuwa, lakini nimegundua kwamba taswira ya mwanzo inaweza isiwe sawa na taswira ya mwisho ambayo Mungu ameichora kwa ajiri yangu.
Ndoto inaweza kuwa ibada ya sanamu. Hii inatokea tunapoweka tumaini letu katika kitu cha kuchongwa na mawazo yetu. Inaweza kuwa rahisi zaidi kuweka tumaini letu katika kitu tusichokiona na kukitawala, kuliko kukiweka kwa Mungu ambaye hatuwezi kumuona na kumtawala.
Ushirika wa kweli na urafiki wa karibu unaweza kuwa unatisha. Uponyaji unaweza kuwa unatisha. Mambo haya yanahitaji uaminifu na ujasiri kutembea na Mungu katika njia ngeni kwa namna ambayo hatujawaza. Lakini Mungu, Mungu wetu, anataka kwenda nasi katika safari hii. Atasawazisha sehemu ngumu kuwa laini na kuleta mwanga pasipokuwa na mwanga.
Kama tutaruhusu mwanga wa Mungu kuingia mioyoni mwetu, anaweza kufunua chanzo halisi ya maumivu yetu, ili uponyaji uweze kutokea. Ni hapo tuu tutakapoweza kuona wazi kilichotufanya kukwepa katika ndoto. Ndipo tutakapoweza kusalimisha taswira ya maisha yetu kwa Mungu mwema, tukijua kwamba aweza kufanya zaidi, kuliko tuyaombayo, tuyawazayo au kufikiria!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Tunafanyaje wakati ndoto zetu zinapoonekana kuwa haziwezi kutimia? Ukiwa umeshinda matusi na hofu, pamoja na kuvunjika moyo baada ya ndoa kuvunjika, ninakabiliwa na swali mara kwa mara. Ikiwa unapitia uharibifu wa tukio au hasara, au kuchanganyikiwa baada ya kusubiri jambo kwa muda mrefu, ndoto ya Mungu kwa maisha yako bado iko hai! Rafiki ni wakati wa kuwa na ndoto tena.
More