Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kukombolewa kwa ndotoMfano

Dreams Redeemed

SIKU 7 YA 7

Kuna mstari katika maombi ya faragha ambao mara nyingi unaimbwa katika hatua 12 za mikutano ambayo inamuomba Mungu atusaidie kukubali "magumu kama njia kuelekea kwenye amani; tukiichukua kama Yesu alivyofanya, ulimwengu huu wa dhambi kama ulivyo, siyo kama nilivyotarajia".

Mstari huo siku zote ulinigonga kwa sababu nguvu yangu nyingi niliitumia kujaribu kutatua na kudhibiti mazingira na watu wanaonizunguka ili kutengeneza maisha kama nilivyotaka yawe...kujitahidi kufanya ndoto zangu zitimie. Hakika sikufanikiwa.

Matokeo ya talaka yangu, nilipoteza nyumba yangu, mkopo wangu uliathirika, na nilijisikia kama, moja baada ya nyingine, nyavu zote za usalama nilizojiwekea, na maisha niliyokuwa najaribu kujenga yaliharibika moja kwa moja. Maisha hayakuwa kama ambavyo nilitaka.

Wakati fulani, nilijikuta naomboleza na kulia kwa Mungu, " Haikuwa kama nilivyotegemea". Mungu alisikia. Halafu, alisema na moyo wangu.

Nilikuokoa.

Upuuzi wa maneno haya ilikuwa kichekesho. Kulikuwa hakuna chochote cha niliyokuwa nayapitia ambacho hata kwa mbali kilionekana kama kuokolewa.

Harmony, nilikuokoa kutoka kwenye tafsiri ya ndoto yako...nitaikoa ndoto.

Ahadi hii, kwamba Mungu ataokoa ndoto, kwamba atarejeza familia kwangu, ilinipa tumaini kwamba majira niliyokuwa hayatadumu milele.

Ninamjua Mungu kuwa mkombozi. Kwanza, alikomboa habari ya maumivu yangu na unyonyaji na anaitumia kuwafikia wengine kupitia Hazina. Leo, miaka mingi baada ya talaka, ninaweza kukwambia kwamba amekomboa ndoto yangu ya kurejeza familia. Mwezi wa Machi 2014, niliolewa na mwanaume bora aliye wa ajabu, mwenye upendo, baba wa pili kwa binti yangu mzuri! Januari 2018, nilipata mtoto mzuri wa kiume ambaye ameleta furaha sana nyumbani mwetu.

Ninapenda habari ya Yusufu, kwa sababu ni mfano wa muota ndoto aliyemwamini Mungu, hata lipoonekana kwamba ndoto zake zote zilikuwa zimepotea. Alisalitiwa na familia, aliachwa, kachukuliwa utumwa, kafungwa, na kusahaulika. Katika hayo yote, Mungu alikuwa na Yusufu. Mwishowe, ukweli wake katika Mungu ulimuwezesha kupanda juu zaidi ya mazingira yake na kuokoa familia yake na Wamisri wote na njaa. Mugu alitumia kila hatua ya maisha ya Yusufu na habari yake kwa wema! Mungu alikomboa ndoto.

Najiuliza kama Yusufu aliwahi kufikiria kuiacha ndoto? Badala yake, alibaki mwaminifu wakati wote wa majira na mazingira yake, alimruhusu Mungu amtumie, na aliendelea kuota. Taifa liliokolewa kwa sababu ya uaminifu wake.

Sielewi unapitia nini. Sijui majaribu au mashambulizi ambayo Mungu anaotea maisha yako yamepotea. Lakini ninajua hili, --Mungu ni mkombozi. Yeye ni mwaminifu. Unapoendelea kuota, kuendelea kumtumaini, endelea kuvumilia… 

Mungu atakomboa ndoto.

 

Ujumbe kutoka kwa Harmony:

Naamini umefurahia ibada hii! Ningependa kuendelea kukutia moyo kuishi kwa uhuru, kuota ndoto kubwa, na kufanya mema! Ninakualika kuangalia blogu yanguhttps://harmonygrillo.com/">www.HarmonyGrillo.com. Kujifunza mengi kuhusu Hazina, unaweza kuangalia https://www.iamatreasure.com/">www.iamatreasure.com

 

B
siku 6

Kuhusu Mpango huu

Dreams Redeemed

Tunafanyaje wakati ndoto zetu zinapoonekana kuwa haziwezi kutimia? Ukiwa umeshinda matusi na hofu, pamoja na kuvunjika moyo baada ya ndoa kuvunjika, ninakabiliwa na swali mara kwa mara. Ikiwa unapitia uharibifu wa tukio au hasara, au kuchanganyikiwa baada ya kusubiri jambo kwa muda mrefu, ndoto ya Mungu kwa maisha yako bado iko hai! Rafiki ni wakati wa kuwa na ndoto tena.

More

Tungependa kumshukuru Harmony Grillo (I Am A Treasure) kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: http://harmonygrillo.com