Kukombolewa kwa ndotoMfano
Sikudhani nitaishi kuiona ishirini na moja. Baada ya historia ndefu ya unyanyasaji wa kijinsia, kubakwa, na kuishi katika mazingira magumu, mama yangu aliniacha peke yangu katikati ya majirani wabaya, katika umri wa miaka kumi na tatu, na mdogo wangu wa miaka nane, kujitafutia kwa miezi mitatu. Wakati ule wa kiangazi, nilijihusisha na kijana ambaye alijitolea kutupa chakula na kutulinda. Mahusiano yalikuwa ya unyanyasaji na unyonyaji, na baadaye yaliniongoza kuingia kwenye biashara ya ngono. Kimsingi, huyo rafiki yangu wa kiume akawa ndiye mmiliki wangu na maisha yakawa hayawezekani tena.
Ingia Yesu.
Ndani yake, nilipata neema, uponyaji, na njia ya uhuru. Nilianza kuota tena. Niliota juu ya siku nitakapokuwa na nyumba nyeupe yenye uzio mweupe, bustani ya majani ya kijani na michezo ya watoto ikiwa imetapakaa kila sehemu. Niliota juu ya familia iliyokuwa pamoja ambayo wote tulikuwa na jina moja la ukoo. Ndoyo yangu iliwakilisha usalama na utulivu--kitu ambacho sikukipata katika maisha yangu yote ya utotoni.
Nilikose kuamini kwamba kama nitakwenda kanisani kila jumapili, kusoma vitabu sahihi, na kufanya mambo sahihi, ndoto zangu zote zitatimia na nitakuwa na kinga fulani ya Yesu kwenye masumbufu ya maisha.
Ndani ya miaka michache, kila kitu kilikuwa kinaenda kama nilivyopanga. Niliolewa na mtoto mzuri, na nilikuwa na nyumba yenye nafasi. Maisha yalikuwa mazuri mpaka nikawa najionea wivu mwenyewe!
Nilipogundua kwamba mume wangu ana mahusiano, na mwishowe sikuwa tayari kupigania kuirejesha ndoa yetu, nilijisikia kana kwamba kila tumaini nililokuwa nalo kwa maisha yangu limevunjika. Maisha niliyokuwa nayaota sasa yanasambaratika.
Katika shairi lake, “Harlem”, Langston Hughes anauliza swali. “Kunatokea nini kwenye ndoto iliyoahirishwa?”
“Je, inakauka
kama zabibu juani?
Au usaha kwenye kidonda—
Halafu kimbia?”
Naamini kinachotokea kwenye ndoto zetu zinapoahirishwa, hazitimii, au hata kuvunjika, inategemea na muotaji. Jinsi tunavyopokea kunategemea kama tunasukumwa karibu na ndoto ya Mungu kwa maisha yetu au mbali nayo.
Katika ukiri wa mume wangu, nilikabiliwa na uamuzi…
Nitaweka wapi tumaini langu? Nitaweka kwenye ndoto niliyoota juu ya maisha yangu? Au nitaweka tumaini langu kwa Mungu?
Kukingana na Biblia, ndoto iliyoahirishwa hufanya moyo kuugua, lakini tumaini katika Yesu ni nanga kwa ajili ya roho yetu. Sikuweza kubadilisha mazingira yangu, kama nilivyotaka, lakini ningeweza kuamua jinsi nitakavyolipokea.
Ninakukaribisha utafakari katika maswali yafutayo: Tumaini lako liko wapi leo? Je, tumaini lako liko kwenye ndoyo ya maisha yako? Au tumaini lako liko kwa Mtoa Ndoto?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Tunafanyaje wakati ndoto zetu zinapoonekana kuwa haziwezi kutimia? Ukiwa umeshinda matusi na hofu, pamoja na kuvunjika moyo baada ya ndoa kuvunjika, ninakabiliwa na swali mara kwa mara. Ikiwa unapitia uharibifu wa tukio au hasara, au kuchanganyikiwa baada ya kusubiri jambo kwa muda mrefu, ndoto ya Mungu kwa maisha yako bado iko hai! Rafiki ni wakati wa kuwa na ndoto tena.
More