Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mt 20:29-33

Mt 20:29-33 SUV

Hata walipokuwa wakitoka Yeriko mkutano mkubwa wakamfuata. Na tazama, vipofu wawili wameketi kando ya njia, nao waliposikia ya kwamba Yesu anapita, walipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Bwana, mwana wa Daudi! Mkutano wakawakaripia, wanyamaze. Lakini wao wakazidi kupaza sauti, wakisema, Uturehemu, Bwana, mwana wa Daudi! Yesu akasimama, akawaita, akasema, Mnataka niwafanyie nini? Wakamwambia, Bwana, twataka macho yetu yafumbuliwe.