Soma Biblia Kila Siku 11Mfano
Mwimbaji anazingatia historia ya Israeli. Anakumbusha kwamba Mungu pekee huweza kumwokoa mwanadamu katika matatizo yake. Tangu ujana wa taifa la Israeli huko Misri, Waisraeli waliteswa (m.1). Lakini Mungu alikata kamba zilizowafunga utumwani, na kuwaweka huru, kwa sababu BWANA ndiye mwenye haki (m.4). Ila bado maadui wanatafuta kuwatesa. Kwa hiyo mwimbaji anamwomba Mungu afanye maadui hao kuwa watu wasiofaa kama nyasi zinazokauka katika jua. Katika mapito yetu, tumtegemee Mungu, kwani yeye hujishughulisha na maisha yetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz