Soma Biblia Kila Siku 11Mfano
Wampendao (m.28) au wateule wa Mungu (m.33) ni wale waliokubali kutubu na kumwamini Yesu Kristo kama Mwokozi wao. Ndugu msomaji, kama wewe ni mmoja wao, maneno ya somo hili ni kwa ajili yako ili kukufariji na kukutia moyo! Ukiwa ndani ya Yesu Kristo usiwe na mashaka! Wanaolichukia jina la Yesu Kristo wanaweza kutuudhi na hata kutuua, lakini hawawezi kutuondolea wokovu wetu!Tunao ushindi, maana tuko ndani yake aliyeshinda. Maana ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea(m.34). Katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda(m.37). Yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu(m.39). Mungu Mwenye Enzi Yote ametuhesabia haki katika Yesu Kristo (m.33)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz