Soma Biblia Kila Siku 11Mfano
Leo na kesho tunasoma juu ya matukio ya pekee yaliyotokea katika maisha ya Daudi. Ni hadithi nzuri ya kuvutia. Huyo tajiri Nabali alikuwa akiwakata manyoya kondoo zake huko Karmeli (m.2). Wakati wa kufanya hivyo ilikuwa desturi kufanya karamu. Na kama ni tajiri, ilikuwa mila yao kwamba maskini na wengine wenye mahitaji katika eneo lake wasaidiwe. Hivyo kimila Daudi alikuwa na haki kabisa kuomba msaada kwa Nabali. Tena Daudi alikuwa amewatendea watumishi wake mema sana huko nyuma, kama anavyomwambia Nabali katika m.7,Wachungaji wako wamekuwa pamoja nasi, wala hatukuwadhuru, wala hawakukosa kitu wakati wote walipokuwako huko Karmeli.Tafakari pia jinsi kijana mmojawapo alivyompasha habari Abigaili, mkewe Nabali, akisema,Watu hawa walitutendea mema sana, wala hatukupata dhara, wala sisi hatukupotewa na kitu cho chote, wakati wote tulipofuatana nao, tulipokuwako mavueni; watu hao walikuwa boma kwetu usiku na mchana, wakati wote tulipokuwa nao tukiwachunga kondoona (m.14-16). Lakini ajabu, Daudi akakataliwa!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz