Soma Biblia Kila Siku 11Mfano
Daudi alizidi kupata ushindi, na Sauli akazidi kuaibishwa. Sauli alipotambua Mungu alivyokuwa amemlinda Daudi mle pangoni na Daudi alivyomhurumia, akalia. Akamwambia Daudi, Wewe u mwenye haki kuliko mimi; maana wewe umenitendea mema, nami nimekutenda mabaya (v.17). Roho hii aliyoonyesha Daudi siku hiyo ni roho ya ajabu. Ni roho ya Kristo. Yesu anaitwa Mwana wa Daudi (Mt 21:9). Katika maisha yake, Yesu alionyesha roho kama babu yake Daudi. Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume.Yesu akajibu akasema, Mwe radhi kwa hili. Akamgusa sikio, akamponya(Lk 22:50-51). Walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, ndipo walipomsulibisha [Yesu], na wale wahalifu, mmoja upande wa kuume, na mmoja upande wa kushoto. Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo(Lk 23:33-34). Je, msomaji, una roho hii ya Kristo? Jipime kwa neno lifuatalo kutoka katika Rum 12:17-21: Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz