Soma Biblia Kila Siku 11Mfano
Waisraeli walimhesabu Paulo kama adui wao, maana aliwatetea watu wa Mataifa kuwa kwa kumwamini Kristo wataweza kuwa watoto wa Mungu bilakutahiriwa na kufanywa Waisraeli. Hivyo alihitaji kuwashuhudia upendo wake kwa Waisraeli (ndivyo alivyofanya katika somo la jana, yaani, m.1-5). Na leo anajitetea kutokana na neno la Mungu: Si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao (m.8). Tangu awali Mwisraeli wa kweli ni yule wa ahadi. Esau hakuwa mtoto wa Mungu ingawa ni wa ukoo wa Ibrahimu! Maneno mengine ya Biblia yanayothibitisha hiyo, kwa mfano Yohana mbatizaji anavyosema katika Lk 3:8, Toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto. Fikiria pia Paulo alivyoandika katika Gal 3:26-29: Ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz