Soma Biblia Kila Siku 11Mfano
Heri kila mtu amchaye BWANA (m.1). Ni nini maana yake? Heri ni sawa na kuwa na amani, neema, baraka, ustawi n.k. Na amchaye BWANAndiye mtu anayemwamini BWANA na kumtii. Maisha yetu yakionyesha kumtegemea BWANA namna hiyo, hatutafanya kazi bure. Taabu ya mikono yako hakika utaila; utakuwa heri, na kwako kwema(m.2). Tutafurahia baraka za BWANA katika familia zetu, na katika kanisa letu. Bidii yetu yote ilenge uheri hapo (zingatia m.5 unavyosema kuhusu Yerusalemu, mahali walipokusanyika waumini kumwabudu Mungu: BWANA akubariki toka Sayuni; uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako). Je, wewe unamcha BWANA? Tafakari.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz