Soma Biblia Kila Siku 11Mfano
Basi ni vivi hivi wakati huu sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema (m.5). Mtume Paulo mwenyewe (m.1) pamoja na mitume wengine ni sehemu ya mabaki haya, yaani ni Waisraeli waliomfuata Yesu na kukiri kwamba ni Kristo na Mwana wa Mungu. Ni wazi kuwa mitume hao, na hasa Paulo, hawakuwa na matendo ambayo yaliwastahilisha kuitwa na Yesu. Ni kwa neemaya Mungu tu. Na ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema(m.6; kama ukitaka kusoma ushuhuda wa Paulo jinsi neema ya Mungu ilivyoingia maishani mwake, tafuta 1 Tim 1:12-17). Haya kweli yanaonyesha kuwa Mungu hajawasukumia mbali watu wake (m.1), ingawa walio wengi akawaadhibu! Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie, hata siku hii ya leo(m.8).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz