Soma Biblia Kila Siku 11Mfano
Ni mara ya mwisho Daudi na Sauli kukutana. Na tunaona ukuu wa Mungu. Sauli alikuja kumwinda Daudi ili amwue, lakini Mungu akamzuia na kuyageuza mambo kabisa. Ndipo ikambidi Sauli kumtakia Daudi heri badala ya mabaya! Sauli akamwambia Daudi, Ubarikiwe, Daudi, mwanangu; utatenda mambo makuu, tena hakika yako utashinda. Basi, Daudi akaenda zake; Sauli naye akarudi kwao (m.25). Tukio hili linafanana na tukio la Bileamu ambaye Bwana alimlazimisha kuwabariki Waisraeli ingawa yeye alitaka kuwalaani! Mfalme Balaki akamwambia Balaamu, Umenitendea nini? Nimekuleta ili uwalaani adui zangu, na tazama, umewabariki kabisa kabisa.Naye akajibu, akasema, Je! Hainipasi kuangalia, niseme neno lile Bwana atialo kinywani mwangu?(Hes 23:11-12; ukitaka kujua zaidi habari hiyo, soma pia Hes 22:1-6 na 23:5-10).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz