Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11

SIKU 26 YA 30

Nabii Samweli alikuwa amewakusanya Waisraeli wakaonekana kama taifa moja wakiwa na mfalme mmoja. Kwa hiyo Samweli alipokufa (habari yake inapatikana katika 25:1) Israeli wote walikuwa wamemwomboleza (m.3). Alikuwa kiongozi mzuri na mtiifu mbele ya Bwana. Lakini Mungu hakuwaacha Waisraeli bila kiongozi. Samweli alipofariki, kiongozi mwingine mzuri alikuwa yupo mbioni kuupokea uongozi, yaani Daudi, wala si Sauli. Sauli alianza kazi yake vema: Alikuwa amewaondolea mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi (m.3). Ila sasa mwenyewe hulitafuta giza lile alilofukuza kwa jina la Bwana:Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori(m.7).

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11

Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz