Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11

SIKU 29 YA 30

Daudi na watu wake waliporudi nyumbani wakashtuka sana, maana mji wao ulikuwa umechomwa moto, na watu wote wamechukuliwa mateka na Waameleki. Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakainua sauti zao na kulia, hata walipokuwa hawana nguvu za kulia tena(m.4). Hata siku hizi katika maisha ya sisi Wakristo hutokea matukio magumu yanayotufadhaisha sana. Tujifunze kwa Daudi, mtu wa Mungu, namna ya kufanya!. 1. Daudi alizidi kumtegemea Bwana: Daudi alijitia nguvu katika Bwana, Mungu wake (m.6)! 2. Hakumwulizia Mungu sababu ya haya kutokea, bali alimwuliza afanye nini.Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote(m.8)! 3.Akalitii jibu la Bwana! Basi Daudi akaenda, yeye na wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye, nao wakakifikilia kijito Besori, ambapo wale walioachwa nyuma walikaa(m.9). Ukipenda, unaweza kusoma 1 Pet 5:6-11 ambapo sisi tunaambiwa kufanya vivyo hivyo.

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11

Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz