Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11

SIKU 25 YA 30

Basi Daudi akaondoka, yeye na hao watu mia sita aliokuwa nao, akamvukia Akishi, mfalme wa Gathi (m.2). Kwa usalama wake, Daudi akaona ni nafuu kwenda kukaa kwa adui ya Israeli, yaani Wafilisti, kuliko kubaki nyumbani Israeli! Mfalme Akishi alifahamu uhodari wa Daudi akaona itakuwa faida kwake Daudi akiwa mtu wake. Akampa mji wa Siklagi. Daudi alifanya ujanja ili ampendeze Akishi. Aliwashambulia watu ambao ni adui wa Israeli(Kut 17:14, Bwana akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu). Lakini kwa Akishi, Daudi alisema kwamba amewapiga adui wa Wafilisti.Akishi humwuliza, Je! Mmeshambulia upande gani leo? Na Daudi husema, Juu ya Negebu ya Yuda, au, juu ya Negebu ya Wayerameeli, au, juu ya Negebu ya Wakeni. Tena Daudi hakumhifadhi hai mume wala mke ili kuwaleta Gathi, maana alisema, Wasituchongee kusema, Ndivyo alivyofanya Daudi, tena ndivyo ilivyokuwa desturi yake wakati wote alipokaa katika nchi ya Wafilisti(m.10-11)!

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11

Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz