Soma Biblia Kila Siku 11Mfano
Ndipo Akishi akamwita Daudi, akamwambia ... hao wakuu hawakuridhii. Basi sasa urudi, uende zako kwa amani, ili usiwachukize hao mashehe wa Wafilisti (m.6-7). Neno "mashehe" hapa inafaa zaidi kutafsiri "wakuu" au "machifu". Bila shaka Daudi angalifanya kama wale wakuu wa Wafilisti walivyotabiri, Asiende pamoja nasi vitani, asije akawa adui wetu vitani; kwani mtu huyu angejipatanisha na bwana wake kwa njia gani? Je! Si kwa vichwa vya watu hawa?(yaani, vichwa vya Wafilisti; m.4). Daudi asingaliweza kuwa adui kwa wenzake Waisraeli. Ila Akishi alimwamini Daudi, maana Daudi alikuwa amemfanyia ujanja (habari hii unaweza kusoma katika 1 Samweli 27:1-12). Mungu ndiye aliyewapa wakuu hao wa Wafilisti ufumbuzi, maana alitaka kumwadhibu Sauli kwa mkono wao!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz