Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11

SIKU 27 YA 30

Sauli alikwenda kupiga bao, kwa sababu aliwaogopa sana Wafilisti, na kwa sababu Bwana alikuwa hamjibu tena. Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii (28:5). Ndipo Sauli alitafuta msaada kwa mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, akimwambia, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako (28:8), akamwomba ampandishie roho ya marehemu Samweli (28:11). Huyo mwanamke alipofanya hivyo alilia kwa sauti kuu akisema, Naona mungu (yaani roho ya marehemu) anatoka katika nchi (28:13). Habari ambayo Sauli alipata kwa Samweli ilikuwa mbaya sana:Bwana amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi. Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya Bwana, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii Bwana amekutendea hili leo. Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena Bwana atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti(m.17-19). Sauli akaingiwa na hofu kubwa, akielewa kuwa mtu akitaka kufanikiwa kazi ya Mungu kwa nguvu za giza, anamchukiza Mungu na atapata mwisho mbaya! Zingatia ilivyoandikwa katika 2 Kor 6:14-7:1, Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi. Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11

Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz