Soma Biblia Kila Siku 11Mfano
Daudi ni shujaa. Aliingia katikati ya jeshi lenye askari 3000! Bwana alimlinda. Daudi akalitwaa lile fumo, na lile gudulia la maji, kichwani pa Sauli; nao wakaenda zao, wala hapana mtu aliyeliona jambo hili wala kulijua, wala kuamka; maana wote walikuwa wamelala; kwa kuwa usingizi mzito kutoka kwa Bwana umewaangukia (m.12)! Daudi amejifunza sasa kwamba asijilipie kisasi. Kwa hiyo imeandikwa katika m.9-10: Daudi akamwambia Abishai, Usimwangamize [mfalme Sauli]; kwani ni nani awezaye kuunyosha mkono wake juu ya masihi wa Bwana, naye akawa hana hatia? Daudi akasema, Aishivyo Bwana, Bwana atampiga (m.9-10). Sauli aliwekwa kuwa Mfalme na Bwana mwenyewe akimtia mafuta (ndiyo maana ya masihi) kwa mkono wa nabii Samweli. Kwa hiyo Daudi alitegemea kwamba Bwana mwenyewe atamwondoa Sauli kwa wakati wake na kwa njia atakayojua yeye.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz