Soma Biblia Kila Siku 11Mfano
Paulo amemaliza mafundisho yake juu ya mpango wa Mungu kwa Waisraeli; amejaa sifa na shukrani! Anamtukuza Mungu kwa ajili ya njia zake za ajabu! Mungu ni mwaminifu! Kutokana na ahadi zake kwa Ibrahimu, Isaka, Yakobo na manabii, hawezi kuliacha daima taifa lake teule.Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake(m.29). Tuna bahati, sisi tuishio leo, maana twaona ahadi hizi zikitimizwa mbele ya macho yetu! Waisraeli wamepewa tena nchi yao ya ahadi (mwaka 1948), na wanazidi kurudi kwa wingi kutoka dunia nzima! Tafakari ahadi ya Mungu katika Yer 23:5-8:Tazama siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi.Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu. Kwa hiyo, angalia, siku zinakuja, asema Bwana, ambapo hawatasema tena, Aishivyo Bwana, aliyewatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri;lakini, Aishivyo Bwana, aliyewapandisha na kuwaongoza wazao wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi zote nilikowafukuza; nao watakaa katika nchi yao wenyewe.Bwana yu karibu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz