Soma Biblia Kila Siku 11Mfano
Je, wamejikwaa hata waanguke kabisa? (m.11). Je, Waisraeli wametupwa na Mungu moja kwa moja bila uwezekano wa kukubaliwa tena? Huenda Wakristo wa Tanzania tungejibu, "Ndiyo"? Au tuna mawazo gani juu yao? Afadhali tukubali kuongozwa na jibu la Paulo ili tuwe katika ukweli wa Mungu!Jibu lake ni "Hasha"! Maana ya Shinakatika m.16-18 ni Kristo. Mti wa mzeituni ulio mwema ni watu wa Mungu. Awali ulikuwa ni Waisraeli; kwa sasa ni Wakristo na Wayahudi wale wanaomwamini Yesu kuwa ni Masihi (=Kristo) wao. Mzeituni mwitu ni watu wasio Waisraeli kwa asili, yaani sisi wa Mataifa mengine. Kwa hiyo tusijivune! Rudia m.17-21.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz