Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11

SIKU 16 YA 30

Tunafikiri Mungu ni kama sisi. Sisi tukikosewa na mtu, hatuwezi kumsamehe hivi hivi tu. Lazima afanye tendo la upatanisho. Sasa sisi tumemkosea Mungu. Yeye pia anataka tendo la upatanisho lifanyike. Ila haki yake ni tofauti na haki yetu(ling. ”haki ya Mungu” katika m.3 na ”Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki” katika m.4)! Maana Mungu alipoona kuwa sisi tumeshindwa kutenda tendo la upatanisho la kumridhisha, akaamua mwenyewe kwa upendo wake kutenda tendo hili kwa mwana wake! Na tulikuwa hatujamwomba. Ndivyo tunavyokumbushwa katika m.20 ambapo neno la Mungu katika Isa 65:1 linanukuliwa:Nalipatikana nao wasionitafuta, nalidhihirika kwao wasioniulizia. Maana Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi(5:8)! Haya si mambo ya kawaida, bali ni mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao(1 Kor 2:9). Kwa hiyo tunahitaji kuyasikia tena na tena na tena – kama tunavyokumbushwa katika m.17: Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11

Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz