Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11

SIKU 15 YA 30

Paulo alitaka sana Wayahudi waokoke. Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa(m.2). Huko nyuma Paulo mwenyewe alikuwa namna iyo hiyo. Aliwaudhi Wakristo kwa sababu alikuwa na juhudi kwa ajili ya Mungu! Ila hakuwa na maarifa. Ni kipofu. Hakumtumikia Mungu bali alimwudhi Mungu. Mwenyewe anashuhudia katika Matendo 22:3-8 alivyofanya kabla hajampokea Yesu: Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi; nikawaudhi watu wa Njia hii hata kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume na wanawake. Kama Kuhani Mkuu naye anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipokea barua kwao kuwapelekea ndugu wale, nikaenda Dameski, ili niwalete wale waliokuwa huko hata Yerusalemu, hali wamefungwa, ili waadhibiwe. Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote. Nikaanguka nchi, nikasikia sauti ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi? Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi. - Kumbe, mtu anaweza kuwa na juhudikwa ajili yaMungu bila kuwa mtoto wa Munguna bilakuwa mwenye haki mbele yake! Tukubali kuokoka kwa neema. Tumkubali Yesu. Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka(m.9)!

siku 14siku 16

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11

Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz