Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11

SIKU 14 YA 30

Vyombo vya ghadhabu (m.22) ni Waisraeli. Hao ni taifa teule waliotendewa kila tendo jema na Mungu, lakini wakawa na mioyo migumu wakazifuata njia zao wenyewe. Mungu aliwavumilia sana! Kwa uamuzi wake hata mwana wake akazaliwa katika taifa hili! Lakini wakamwua! Sababu inaonekana katika m.31-32: Israeli wakiifuata sheria ya haki hawakuifikilia ile sheria.Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuifuata kwa njia ya imani, bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Kwa hiyo walijikwaa juu ya Yesu. Vyombo vya rehema (m.23-24) ni watu wa Mataifa waliomwamini Yesu (m.25-26) - pamoja na Waisraeli wachache ambao wanaitwa mabakikatika m.27 na uzaokatika m.29. Tuseme nini, basi? Ya kwamba watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani(m.30). Hivyo Mungu ametufunulia ghadhabu yake, uweza wake na utukufu wake, ilivyoelezwa katika m.22-23: Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kuudhihirisha uweza wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu; tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu.

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11

Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz