Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11

SIKU 13 YA 30

Baada ya kila fundisho Paulo anauliza swali la udadisi ambalo anajua Wayahudi wangeuliza. Leo anaelezea mambo ambayo yanapitaufahamu wa binadamu: Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi (m.20)? Kwa hiyo jambo muhimu kwa Paulo si kuiridhisha akili ya binadamu kwa kila jambo. Bali la muhimu zaidi ni kuonyesha msingi wa kila fundisho katika Maandiko Matakatifu(angalia m.15 na 17 kuhusu anavyothibitisha aliyoandika:Maana [Mungu]amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. … Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote). Fundisho: Kuokoka kunategemea neema ya Mungu tu (m.16: Si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu)!

siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11

Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz