Soma Biblia Kila Siku 11Mfano
Katika Warumi sura ya 9-11 Mtume Paulo anafundisha juu ya mpango wa Mungu kwa taifa la Israeli, taifa teule la Mungu. Hao walimkataa Kristo ingawa wao ndio wangalikuwa wa kwanza kumpokea (ling. jinsi Waisraeli wanavyosifiwa katika m.4-5 kuwawenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake; ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Tafakari pia Paulo anavyoandika kuhusu Injili katika 1:16 kwamba ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia)! Na hili ni taifa lake Paulo kwa jinsi ya mwili,yaani, kutokana na ukoo wake, kama anavyoeleza katika 11:1,Mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya Benyamini. Uchungu wake kwa ajili yao umepita kiwango, maana anasema, Nina huzuni nyingi na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu.Kwa maana ningeweza kuomba mimi mwenyewe niharimishwe (yaani kulaaniwa) na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu (m.2-3). Hii ni roho ya Kristo! Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti(Gal 3:13). Katika 1 Petro 2:21 Petro anatukumbusha kuwa habari hiyo ina maana maradufu kwetu: Kristo aliteswa (1) kwa ajili yenu, (2) akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz