Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11

SIKU 6 YA 30

Naye Sauli alikuwa akimtafuta kila siku, lakini Mungu hakumtia mikononi mwake (m.14). Mungu akimlinda mtu mwanadamu, hata akifanya nini, hawezi kumdhuru, maana Mungu ni mkuu. Mbele yake hata nguvu ya mapepo au wachawi inashindwa. Tunaona Mungu alivyomtia Daudi moyo kwa kupitia rafiki yake na muumini mwenzake Yonathani. Yonathani, mwana wa Sauli, akainuka akamwendea Daudi huko Horeshi, akamtia nguvu mkono wake katika Mungu. Akamwambia, Usiogope, kwa maana mkono wa Sauli, babangu, hautakupata; na wewe utakuwa mfalme juu ya Israeli; na mimi nitakuwa wa pili wako; ndivyo ajuavyo hata Sauli, babangu. Na hao wawili wakafanya agano mbele za Bwana (m.16-18). Biblia ya Habari Njema inasema, Akamtia moyo kwamba Mungu anamlinda. Ndivyo tunavyotakiwa kupendana na kutiana moyo sisi Wakristo! Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu; kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi. Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani(Rum 12:10-14).

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11

Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz