Soma Biblia Kila Siku 11Mfano
Abigaili, mke wake Nabali, alikuwa na tabia tofauti kabisa na mume wake. Kwa tendo lake la busara akawa chombo cha Mungu kuzuia mambo mawili mabaya: 1) Aliokoa maisha yake mwenyewe pamoja na watu wote wa nyumba ya Nabali (kama Daudi alivyomwambia Abigaili katika m.34, Ni kweli, aishivyo Bwana, Mungu wa Israeli, aliyenizuia nisikudhuru, kwamba hungefanya haraka kuja kunilaki, hakika huyu Nabali asingaliachiwa hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi). 2) Pia Abigaili alimwokoa Daudi kwamba asijilipie kisasi kwa mkono wake mwenyewe (Daudi mwenyewe alimwambia Abigaili hivyo katika m.33, Ibarikiwe busara yako, na ubarikiwe wewe, uliyenizuia hivi leo nisimwage damu, wala kujilipiza kisasi kwa mkono wangu mwenyewe). Katika Rum 12:19 tunaambiwa tuzingatie hiyo,Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Daudi hakuwa Kristo, bali ni mwanadamu tu mwenye makosa yake. Kosa siku ile lilikuwa kwamba aliamua kuondoka kwa hasira ili amwue Nabali na jamaa zake, bila kwanza kumwuliza Mungu (m.12-13).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz