Soma Biblia Kila Siku 11Mfano
Basi mfalme akamwambia Doegi, Geuka wewe, ukawaangukia hao makuhani. Basi, Doegi, Mwedomi, akageuka, akawangukia makuhani, akaua siku ile watu themanini na watano wenye kuvaa naivera ya kitani (m.18). "Naivera ya kitani" ni mavazi ya ukuhani. Ni kama wachungaji au mapadri Tanzania wanavyovaa joho, stola na kola. Watumishi wengine wa Sauli walikataa kuwaua makuhani. Imeandikwa katika m.17, Mfalme akawaambia askari walinzi waliosimama karibu naye Geukeni, mkawaue hao makuhani wa Bwana, kwa sababu mkono wao u pamoja na Daudi, na kwa sababu walijua ya kuwa amekimbia, wasiniarifu. Lakini watumishi wa mfalme walikataa kunyosha mkono na kuwaangukia makuhani wa Bwana. Lakini Doegi akakubali! Kwa kweli ukaidi wa Sauli ulizidi kipimo! Kwa kutenda ujeuri huo Sauli alionyesha wazi anatawaliwa na mapepo mabaya!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz