Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11

SIKU 2 YA 30

Akakimbia siku ile kwa hofu ya Sauli (m.10). Daudi hakuwa na raha. Alikuwa hatarini kila mahali. Akakimbia huko na huko. Hata kwa Wafilisti, maadui wao, akaona ni nafuu kukaa kuliko kwa Waisraeli! Maelezo kidogo kwa habari zinazoweza kuwa ngumu kuelewa: Nobu (m.1) ni mji wa kabila la Walawi. Ulikuwa upande wa kaskazini wa Yerusalemu, na wakati huo Hema ya kukutania ilikuwepo hapa. Mikate mitakatifu (m.4) iliruhusiwa kuliwa na makuhani tu, kama Mungu alivyomwagiza Musa katika Law 24:5-9, Utatwaa unga mwembamba, na kuoka mikate kumi na miwili ya huo unga; sehemu za kumi mbili za efa, zitakuwa katika mkate mmoja. Nawe iweke mistari miwili, mikate sita kwa kila mstari, juu ya hiyo meza safi, mbele za Bwana. Nawe utatia ubani safi juu ya kila mstari, ili uwe ukumbusho kwa hiyo mikate, sadaka ya kusongezwa kwa Bwana kwa moto.Kila siku ya Sabato ataipanga mbele za Bwana daima; ni kwa ajili ya wana wa Israeli, agano la milele. Nayo itakuwa ya Haruni na wanawe; nao wataila katika mahali patakatifu; kwa sababu kwake ni takatifu sana katika sadaka zisongezwazo kwa Bwana kwa moto, kwa amri ya milele. Kuhani akampa ile mikate mitakatifu (m.6). Katika Mt 12:1-8 Yesu alisifu tendo hili kama mfano wa huruma kwa mhitaji!

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11

Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz