Soma Biblia Kila Siku 7Mfano
Katika kitabu cha Mithali, nyakati nyingine neno “hekima” humaanisha Mungu, kama inavyoonekana katika maneno ya leo. Wamtegemeao Mungu hustawi, kama vile Mungu mwenyewe na hekima yake ni mti wa uzima. Linganisha m.18 na Zaburi 1:1-3, Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye↔ Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. Kwake ashikamanaye na Mungu kuna ustawi wa kiroho na kimwili. Tambua kuwa Mungu ndiye aliyeviumba vitu vyote pamoja na sisi. Kwa hiyo anazo baraka tunazohitaji, na ulinzi wote tunaoutumaini. Anaweza kututegemeza na kutuondolea hatari zote! Tumtegemee!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz