Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 7Mfano

Soma Biblia Kila Siku 7

SIKU 20 YA 31

Wakili wa sheria ("msemi mmoja") wa Wayahudi alisema maneno mazuri ili wajipendekeze kwa Feliki (m.2-4:Kwa kuwa mnapata amani nyingi chini yako, Feliki mtukufu, na kwa maangalizi yako mambo mabaya yanatengenezwa kwa ajili ya taifa hili, basi tunayapokea kila wakati na kila mahali, kwa shukrani yote. Lakini nisikuudhi zaidi, nakusihi utusikilize maneno machache kwa fadhili zako). Hili linaonyesha kwamba si watu wa kupenda kweli maana walimchukia! Ndipo wakamshitaki Paulo (Kiswahili cha kisasa): Tumegundua kwamba mtu huyu ni wa hatari mno. Yeye huanzisha ghasia kati ya Wayahudi kila mahali duniani na pia ni kongozi wa kile chama cha Wanazareti. Tena alijaribu kulikufuru hekalu ... (m.5-6). Ukweli ni kwamba walioanzisha ghasia hizo ni Wayahudi, wala hekalu hakulikufuru (17:5,Wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini. Na m.13:Wayahudi wa Thesalonike walipopata habari ya kwamba neno la Mungu linahubiriwa na Paulo hata katika Beroya, wakaenda huko nako wakawachafua na kuwafadhaisha makutano. Pia katika 21:28-29 wanafanya vivyo hivyo)!

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 7

Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.

More

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz