Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 7Mfano

Soma Biblia Kila Siku 7

SIKU 18 YA 31

Mjomba wake Paulo akasikia habari za kuotea kwao(m.16). Tafsiri iliyo sahihi ni: "mtoto wa dada yake" badala ya "mjomba wake". Akaenda akaingia ndani ya ngome akampasha Paulo habari (m.16). Inaonekana Paulo alikuwa na namna fulani ya uhuru huko ndani ya ngome (24:23, [Feliki] akamwamuru yule akida kwamba Paulo alindwe; ila awe na nafasi, wala asimkataze mmojawapo wa rafiki zake kumtumikia). Hiyo ni kwa sababu ya yule jemedari yaani mkuu wa jeshi kujulishwa kuwa Paulo ni Mrumi. Kwa hiyo kufuatana na sheria za Warumi ilikuwa lazima atendewe kwa heshima zaidi na hawakuruhusiwa kumpa adhabu kabla ya kesi yake kuhukumiwa. Walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paulo akamwambia yule akida aliyesimama karibu, Je! Ni halali ninyi kumpiga mtu aliye Mrumi naye hajakuhumiwa bado? Yule akida aliposikia, akaenda akamwarifu yule jemadari, akisema, Unataka kufanya nini? Kwa maana mtu huyu ni Mrumi. Jemadari akaja, akamwuliza, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndiyo. Jemadari akajibu, Mimi nalipata wenyeji huu kwa mali nyingi. Paulo akasema, Na mimi ni Mrumi wa kuzaliwa. Basi wale waliokuwa tayari kumwuliza wakaondoka wakamwacha. Na yule jemadari naye akaogopa, alipojua ya kuwa ni Mrumi, na kwa sababu amemfunga(22:25-29).

siku 17siku 19

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 7

Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.

More

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz