Soma Biblia Kila Siku 7Mfano
Ndugu msomaji, ukiwa mfuasi wa Yesu ujipe moyo na kuvumilia hata kama utajaribiwa na kuona taabu nyingi kwa ajili ya jina lake. Uzidi tu kujikabidhi kwake na kumtegemea. Ndipo utaona kwamba Bwana Yesu hutimiza ahadi yake kama alivyosema: Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, naam, mpaka mwisho wa nyakati; (Mt 28:20, Kiswahili cha kisasa). Ndivyo Paulo alivyopata kuona siku hiyo: Usiku ule Bwana akasimama karibu naye, akasema, Uwe na moyo mkuu; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia habari zangu Yerusalemu, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi nako(m.11)! Sidhani kama utapata ufunuo kama huu wa Paulo ila kwa namna moja au nyingine atakuthibitisha! Ukitaka kufahamu zaidi kuhusu Yesu anavyotoa wito na kuwa pamoja na wale wanaouitikia, soma Mathayo 10:16-20 na 1 Petro 5:6-11!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz